Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA
Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA, Mashindano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2024 yanaendelea kuleta msisimko kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Katika mchakato wa kufuzu kwa mashindano haya, mataifa yanajiandaa kwa mechi muhimu zitakazoamua ni timu gani zitawakilisha ukanda wa CECAFA kwenye mashindano ya CHAN mwaka 2024.
Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA
Hatua ya Kwanza – Raundi ya Kwanza
- Burundi vs Somalia
- Ethiopia vs Eritrea
- Sudan vs Tanzania
- South Sudan vs Kenya
- Djibouti vs Rwanda
Mechi hizi zitaanza kwa mzunguko wa kwanza kati ya tarehe 25 hadi 27 Oktoba 2024, huku mzunguko wa pili ukifanyika kati ya tarehe 1 hadi 3 Novemba 2024.
Hatua ya Pili – Raundi ya Pili
Washindi wa raundi ya kwanza wataingia hatua ya pili kwa kupangiwa kama ifuatavyo:
- Mshindi wa mechi 1 & 2 vs Uganda
- Mshindi wa mechi 3 & 4 vs Mshindi wa mechi 5 & 6
- Mshindi wa mechi 7 & 8 vs Mshindi wa mechi 9 & 10
Hatua hii ya pili ya kufuzu itafanyika kati ya tarehe 20 hadi 22 Desemba 2024 kwa mzunguko wa kwanza, huku mzunguko wa pili ukiwa kati ya tarehe 27 hadi 29 Desemba 2024.
Timu zilizoshinda katika mechi hizi za mchujo zitakuwa zimejihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya CHAN 2024 ambayo itafanyika mwakani.
Mashabiki wa soka wanatarajiwa kushuhudia vita kali za soka kati ya mataifa haya ya CECAFA, huku timu zikijitahidi kupata tiketi ya kuelekea kwenye mashindano ya CHAN.