Michezo

Mwamuzi wa Kariakoo Derby Ametangazwa

Mwamuzi wa Kariakoo Derby Ametangazwa, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtangaza Ramadhan Kayoko, mwamuzi mwenye uzoefu kutoka Dar es Salaam, kuwa atakayesimamia mechi inayosubiriwa kwa hamu, maarufu kama Kariakoo Derby. Mechi hii ya kihistoria kati ya Simba SC na Yanga SC inatarajiwa kupigwa kesho, Oktoba 19, 2024, saa 11:00 jioni, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mwamuzi wa Kariakoo Derby Ametangazwa

Mwamuzi wa Kariakoo Derby Ametangazwa
Mwamuzi wa Kariakoo Derby Ametangazwa “Ramadhan Kayoko”

Ramadhan Kayoko, anayejulikana kwa umahiri wake wa kutafsiri sheria 17 za soka, atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga pamoja na Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba atakuwa Tatu Malogo.

Mashabiki wa mpira wa miguu kote nchini wameshika tama wakisubiri mpambano huu, ambao pia utarushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD. Bodi ya ligi imeweka wazi kuwa maandalizi yote yamekamilika, na hakuna nafasi ya kisingizio kwa timu yoyote.

Kila mmoja anatarajia kuona namna Kayoko atakavyodhibiti mechi hiyo yenye ushindani mkubwa, huku timu zote mbili zikiwa na rekodi za kuvutia msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!