Elimu

Ufadhili Wa Masomo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM)

Ufadhili Wa Masomo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Kampuni ya ALAF Limited inapenda kutangaza ufadhili wa ada kwa wanafunzi watatu (3) waliochaguliwa kusoma Programu ya M.A. Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025.

Ufadhili Wa Masomo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Ufadhili Wa Masomo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
Ufadhili Wa Masomo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Masharti ya Uombaji:

  • Raia wa Tanzania: Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania.
  • Elimu: Awe mhitimu wa Shahada ya Awali katika Kiswahili au programu husika, na kufaulu vizuri katika masomo ya Kiswahili.
  • GPA: Awe na WAKIA (GPA) usiopungua 3.8 wa Digrii ya Kwanza.
  • Udahili: Awe amepata au ameomba udahili katika Programu ya Shahada ya Umahiri katika Kiswahili ya UDSM.
  • Umri: Awe na umri usiozidi miaka 35 wakati analeta maombi.
  • Mahitaji ya Ufadhili: Awe mhitaji wa ufadhili wa ada, na uwezo wa kujigharimia mahitaji mengine kama chakula, malazi, utafiti, na stesheni.

Vitu Vinavyohitajika:

  • Barua ya maombi.
  • Nakala ya Transcript.
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Maelezo mafupi (ukurasa mmoja) yanayobainisha kuhitaji ufadhili wa ada.

Maelezo ya Kuwasilisha Maombi:

Maombi yatumwe kwa:
Mkurugenzi,
Taasisi ya Luma za Kiswahili.
Baruapepe: [email protected]

Tarehe ya Mwisho ya Kupokea Maombi: 25/10/2024

Tafadhali hakikisha unafuata masharti yote ili uweze kujiandikisha kwa ufadhili huu wa ada.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!