Elimu

NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2024

Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Kutangazwa Leo na NECTA. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba kwa mwaka 2024. Matokeo haya yanatarajiwa kwa hamu kubwa na wanafunzi, wazazi, na walimu kote nchini, kwani ni hatua muhimu kwa wanafunzi wanaotamani kujiunga na elimu ya sekondari.

NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2024
NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2024

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2024

Fuata hatua zilizo hapa chini ili kuweza kupata matokeo yako ya Darasa la Saba ya NECTA mtandaoni:

  • Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA: Fungua (https://necta.go.tz), ambayo ni tovuti rasmi ya NECTA.
  • Chagua Menyu: Baada ya kufungua tovuti ya NECTA, tafuta chaguo la menyu katika sehemu ya juu au upande wa menyu kuu.
  • Bofya Kiungo cha Matokeo: Chagua kiungo cha Matokeo na kisha PLSE (Primary Leaving School Examination).
  • Chagua Mwaka wa Matokeo: Utapata matokeo ya miaka yote. Chagua mwaka husika kwa matokeo unayotaka kuona
  • Angalia Tangazo la Matokeo: Kama matokeo yametangazwa, utaona tangazo kwenye tovuti kuhusu matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba.
  • Fungua Tangazo la Matokeo Kamili: Bonyeza tangazo hilo ili kuona matokeo kamili ya mtihani kwa kila eneo.
  • Chagua Mkoa na Wilaya: Baada ya kufungua matokeo, tafuta jina la mkoa wako, kisha chagua wilaya na shule husika ili kuona matokeo ya wanafunzi wa shule hiyo.

BBOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024

Kwa kutumia hatua hizi, utapata matokeo yote unayohitaji kwa urahisi kupitia tovuti ya NECTA.

Kujiandaa kwa Kidato cha Kwanza 2025

Wanafunzi wote waliopata alama zinazotakiwa wataanza rasmi masomo ya sekondari mwaka 2025. NECTA na wizara ya elimu wamepanga mipango madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanajiunga na shule za sekondari bila changamoto yoyote.

Hongera kwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa Darasa la Saba 2024.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!