Elimu

HESLB Majina Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanza kutangaza orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025. Awamu hii ya kwanza inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ya Shahada ya awali, Shule ya Sheria kwa Vitendo na Shahada ya Uzamili.

Wanafunzi kupata taarifa kupitia SIPA

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema wanafunzi wote walioomba mikopo kwa mwaka 2024/2025 wanaweza kupata taarifa za kina kuhusu mikopo yao kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama ‘SIPA’ – Student’s Individual Permanent Account.

HESLB Majina Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB amesema kuwa awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa mwaka 2024/2025 itatangazwa wiki ijayo.

SIPA HESLB TAZAMA HAPA

245,799 kunufaika na mikopo 2024/2025

“Mwaka huu, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 245,799 wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza waliotengewa TZS 284.8 bilioni,’ amesema Dkt. Kiwia na kuongeza kuwa bajeti ya mwaka 2024/2025 imeongezeka kwa TZS 38 bilioni sawa na asilimia 5.1 ikilinganishwa na bajeti ya 2023/2024 iliyokuwa TZS 749.4 bilioni. Mwaka huu pia kiwango cha chini cha mkopo kwa mnufaika mmoja mmoja kimepanda hadi TZS 3.0 milioni kutoka TZS 2.7 milioni mwaka uliopita wa 2023/2024.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!