245,799 Kunufaika Na Mikopo 2024/2025
Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 245,799 wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza waliotengewa TZS 284.8 bilioni. Dkt. Bill Kiwia, Mkurugenzi Mtendaji – HESLB
BAJETI YAONGEZEKA
Bajeti ya mwaka 2024/2025 imeongezeka kwa TZS 38 bilioni sawa na asilimia 5.1 ikilinganishwa na bajeti ya 2023/2024 iliyokuwa TZS 749.4 bilioni. Mwaka huu pia kiwango cha chini cha mkopo kwa mnufaika mmoja mmoja kimepanda hadi TZS 3.0 milioni kutoka TZS 2.7 milioni mwaka uliopita wa 2023/2024
WITO: VYUO KUWASILISHA MATOKEO YA MITIHANI
Kuna vyuo vichache, ambavyo bado havijawasilisha matokeo, tumewakumbusha na tunasisitiza waharakishe kuwasilisha matokeo ili tukamilishe malipo ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na masomo.
WAOMBAJI WA MIKOPO KUPATA TAARIFA KUPITIA ‘SIPA’
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema wanafunzi wote walioomba mikopo kwa mwaka 2024/2025 wanaweza kupata taarifa za kina kuhusu mikopo yao kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama ‘SIPA’ – Student’s Individual Permanent Account.